zone verte

lundi 22 juin 2009

Mila Tu!

Mila Tu, devenir femme maasaï sans l'excision, est le premier documentaire que j'ai co-réalisé avec Charlotte Bruneau. Une longue et belle histoire, qui a dépassé nos attentes!

photo6_mila 

Posté par laulotte à 19:37 - Commentaires [0] - Rétroliens [0]

vendredi 23 janvier 2009

Moyo wangu unalialia… unanikosea bwana

labda ni rahisi zaidi kwa kiswahili
maneno ya lugha yangu yananiumiza bwana

uko wapi sitaki kufahamu
siwezi kuvumilia
siku chache zilizopita
tuliandikiana kama kawaida
lakini ujumbe wako haukuwa wa kawaida
ulikuwepo hospitalini tena
ulichoka sana
ulichoka kupiga vita dhidi ya muda unaokimbia
dhidi ya maradhi
vita vyako havikuwa sawasawa
ulishinda bwana ulishinda

uliota kwenda Amazonia
na sasa ninapoifikiria
amazonia ni Pafu la Dunia
Mapafu yako yalikuwa magonjwa sana
tangu umezaaliwa
hewa ya dunia haikukupendeza
tulijua
tulijua kwamba utaondoka kabla ya mimi
hata kabla ya wazazi wako

leo nabaki kama chizi sivumilii
leo ni siku ya uzaaliwa wako
lakini haupo, haupo

usiku roho yangu inakuita
na leo usiku umekuja tena
ndotoni nakusikia
kama zamani tunavumbua dunia nyingine
kutoka juu ya kilima

mji unanyosha mbele yetu
angalia maisha yanaendelea
ilikuwa wakati wa kiangazi
sasa moyoni mwangu imo masika bila mwisho
jana tena nilikuwepo karibu na kaburi lako
nakutafuta mahali popote

lakini haupo, haupo
ulikuwa na umri miaka thalathini

mapema mno, mapema mno...

Posté par laulotte à 15:33 - Commentaires [1] - Rétroliens [0]